Ijumaa 8 Mei 2026 - 14:15
Tusome Qur’ani | Kwa nini baadhi ya watu hushindwa na kujisalimisha kwa adui katika nyakati za migogoro?

Hawza/ Katika nyakati za migogoro, pale ambapo mwanadamu anakosa kabisa njia na zana zote za dhahiri, huwa na njia chache mbele yake: ima kujisalimisha kwa adui, au kujisalimisha kwa mkondo wa kawaida wa maisha ambao kwa hakika ni aina ya kujisalimisha kwa adui, au kujiua. Lakini kwa mwanadamu alieshikamana na Mungu, hufunguliwa mlango mwingine: mlango wa kumtegemea Mwenyezi Mungu. Mwanadamu alieshikamana na Mungu husema: hapa ni mwisho wa njia, lakini Mungu ninayemjua hupasua hata njia zilizofungwa; kwa upande wa Mungu hakuna kitu kinachoitwa mwisho wa njia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika migogoro na njia zilizofungwa za maisha, mwanadamu asiye na Mungu ana njia tatu mbele yake: kujisalimisha kwa adui, kujisalimisha kwa matukio, au kujiua. Lakini mwanadamu alie na Mungu hufungua mlango wa nne: kumtegemea Mola ambaye hajui mwisho wa njia na ndiye anayefungua njia.

Mfululizo maalumu wa “Tusome Qur’ani” unawasilisha tafsiri za Qur’ani kutoka kwa kiongozi shahidi, ambapo katika toleo hili inachambuliwa mada ya “njia tatu ambazo mwanadamu asiye na Mungu huziona katika hali ya kukata tamaa”, na matini yake inawasilishwa kwenu wasomi.

Je, mmeona baadhi ya watu wanavyofanya wanapokumbana na matatizo ya maisha, katika migogoro, pale ambapo mikono yao imekatika kutoka kwa njia zote za dhahiri? Mmeona? Mmeisikia?

Hufanya moja kati ya mambo kadhaa:

Ima hujisalimisha kwa adui na kusema: kwa kuwa siwezi kufanya chochote, nifanye nini? Hivyo hujisalimisha kwa adui—hiyo ni njia ya kwanza.

Au hujisalimisha kwenye mkondo wa kawaida wa maisha; haendi kujitupa mbele ya adui moja kwa moja, lakini kivitendo huchukua njia na mwenendo fulani, huacha jitihada na harakati, na husahau kwamba kwa hakika amejisalimisha kwenye mkondo wa kawaida wa maisha. Mtu wa aina hii, japokuwa kwa nje hajaonekana kujisalimisha kwa adui, kwa ndani amejisalimisha—hii pia ni hali nyingine ambayo watu wengi huchukua katika migogoro kama hii.

Njia nyingine ni kuhitimisha maisha yao. Yule mtu ambaye anapofikia mamlaka, kwa mfano, huzungukwa na shinikizo na michezo ya nguvu za kimataifa kiasi kwamba huchoshwa kupita kiasi; kila siku kutoka sehemu fulani ya nchi yake kunazuka kelele dhidi yake, na pale anapolazimika kabisa, anapochoka na kukata tamaa, huamua kuhitimisha maisha yake—hujiua.

Hizi ndizo njia ambazo mwanadamu asiye na Mungu huziona katika hali ya kukata tamaa. Unapofika mwisho wa njia, unapofika mahali unapodhani hakuna njia tena, mbele ya watu wa kawaida hufunguka milango kadhaa: mlango wa kujisalimisha—kujisalimu kwa adui, mlango wa kujisalimisha kwenye matukio, mlango wa kujisalimisha kwenye mkondo wa kawaida wa maisha, mlango wa kujiua—kujiangamiza na kujipumzisha na pengine kujuta.

Lakini kwa mwanadamu alie shikamana na Mungu, katika hali ya kukata tamaa hufunguliwa mlango mwingine, ambao kufunguka kwake hufunga milango mingine yote—milango inayoua heshima.

Mlango huo ni upi?

Ni mlango wa kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Husema: hapa ni mwisho wa njia. Lakini anasema: Mungu ninayemjua hupasua hata njia zilizofungwa.

Mwisho wa njia ni nini?

Kwa upande wa Mungu, hakuna mwisho wa njia. Njia zote zilizofungwa hufunguliwa kwa mkono wa uwezo wa Mwenyezi Mungu—kuna njia.

Chanzo: Kitabu Mpango Mkuu wa Fikra za Kiislamu katika Qur’ani, mlango wa Imani, kikao cha 2, ukurasa wa 54

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha